Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) ni shirika lisilo la kiserikali linaloshughulika na masuala ya uelewa na ulinzi wa haki za binadamu na utawala bora. Mojawapo ya kazi zake ni kuandaa ripoti ya kila mwaka ya hali ya haki za binadamu nchini. Ukiwa mmojawapo wa vyanzo muhimu vya taarifa, tunakuomba ujaze dodoso hili. Taarifa hizi zitatumika kuandaa Ripoti ya Haki za Binadamu Tanzania 2019 na si vinginevyo. Tunakushukuru sana kwa ushirikiano wako.
Kuna 26 maswali katika utafiti huu.