Kituo cha sheria na Haki za Binadamu (LHRC) ni shirika binafsi, huru, la hiari, lisilo la kiserikali, lisilofungamana na chama chochote cha kisiasa na lisilotengeneza faida kwa ajili ya kugawana, ambalo linataamali jamii yenye Haki na usawa. LHRC ina lengo la kuwawezesha watanzania kukuza, kuimarisha na kulinda haki za binadamu na utawala bora nchini. Lengo kubwa la LHRC ni kujenga ufahamu wa sheria na haki za binadamu miongoni mwa umma na hasa watu walio kwenye hatari kubwa ya ukiukwaji wa haki zao za msingi, kutoa elimu ya sheria na uraia, kufanya utetezi unaohusisha pia msaada wa kisheria, utafiti na ufuatiliaji wa Haki za binadamu. LHRC ilianzishwa mwaka 1995 na inafanya kazi Tanzania Bara.
Tarehe 26 Septemba 2022, LHRC inaadhimisha miaka 27 tangu ilipoanzishwa na tunaamini kwamba tusingeweza kufika hapa bila msaada wako. Utafiti huu unawataka marafiki wote wa haki waliounga mkono safari hii na wale wanaotarajia kutuunga mkono.
Kuna 16 maswali katika utafiti huu.